Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametoa wito kwa wananchi wote mkoani shinyanga kuacha tabia ya kujihusisha na shughuli za kijamii katika maeneo yote ya hifadhi ya barabara na badala yake waitunze miundombinu hiyo pamoja na alama zake ili iwe endelevu na kwa manufaa ya waliowengi zaidi.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 15 Julai, 2024 wakati akihutubia wajumbe wa waalikwa wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa huku akisisitiza pia wakuu wa taasisi TANROADS na TARURA Mkoa kuhakikisha pia wanasaidia utoaji wa elimu juu ya utunzaji wa miundombinu hii sanjari la kufanya usafi wa mazingira mbele ya maeneo yao wanayoishi au kufanyia shughuli.
"Wananchi, acheni tabia ya kuifuata na kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi ya barabara, badala yake muwe sehemu ya kuitunza, kulinda na kuimarisha miundombinu na alama zake zote ili iwe endelevu na ilete toja iliyokusudiwa na Serikali," amesema RC Macha.
Kando na wito huu, pia RC Macha amewapongeza Wakuu wa Wilaya zote tatu, Mheshimiwa Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga, Kahama na Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya ya Kishapu, Shinyanga, Msalala na Ushetu pamoja na waheshimiwa madiwani wote, wataalam wote wakiongozwa na wakurugenzi wao wote ndani ya Mkoa na wakuu wote wa taasisi zote kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kahakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa yenye kuwaletea maendeleo yenye tija endelevu wananchi katika maeneo yao.
Aidha RC Macha amewashauri wahusika wote wanaohusika na mchakato wa upataikanaji wa wakandarasi kuwa makini zaidi kwani imeinika kuwa baadhi ya wakandarasi ni hawana uwezo mzuri katika utekelezaji wa kazi wanazopewa jambo ambalo linapelekea miradi kuchelewa kukamilika kwa wakati.
Mwisho RC Macha amempongeza sana Eng. Joel Mwambungu ambaye ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga kwa utekelezaji wa maelekezo ya Serikali. Huku Meneja wa TARURA Mkoa wa Shinyanga Eng. Avith Theodory akimshukuru na kumpongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiongeza bajeti ya TARURA katika utekelezaji wa miradi mkoani Shinyanga.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa