• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WA KATA YA KINAGA WAMSHUKURU MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUWAJENGEA KITUO CHA AFYA

Posted on: December 9th, 2023

Na. Shinyanga RS

WANANCHI wa Kata ya Kinaga katika Manispaa ya Kahama mkoani shinyanga wamemshukuru sana Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Kituo cha Afya Kinaga chenye gharama

Zaidi ya wakazi 22,343 wa Kata ya Kinaga na vijiji jirani kunufaika na uwepo wa Kituo cha Afya Kinaga kilichopo Kata ya Kinaga, Manispaa ya Kahama kilichogharimu zaidi ya Tzs. Milioni 669 chanzo cha fedha ni serikali kuu Mil. 500 na Manispaa ya Kahama Mil. 169 kutoka mapato yake ya ndani.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata ya kinaga, Diwani Mhe. Mary Joseph Manyambo alisema kuwa, awali  wananchi wa kata hii walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya Kilomita 15 kwenda Kahama mjini kufuata huduma ya afya ambapo hivi sasa wanapata hapahapa kinaga, hivyo wanamshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha aa ujenzi wa kituo hiki cha afya ambacho kimekuja kuwa mkombozi.

"Tunamshukukuru sana Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ujenzi wa kituo hiki, na leo wananchi wa kinaga wanapata huduma zote muhimu hapahapa kinaga," akisema Mhe. Mary.

Kwa upande wake DC wa Kahama Mhe. Mboni Mhita alimshukuru pia Rais. Mhw. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali wananchi hasa wa kahama ambapo leo wameshuhudia kufunguliwa rasmi kwa kituo cha afya, huku akiwataka wananchi kukitunza na kuwapa ushirkiano qahudumu wa afya kituoni hapo.

Akitoa salamu za mkoa, RC Mndeme amemshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zite hizi ili kuwajengea Kituo hiki na akawashukuru pia manispaa ya kahama kwa kujazia zaidi ya Mil 169 hivyo zaidi ya milioni 669 kugharamia ujenzi huu unaotarajiwa kukamilika Desemba 31, 2023.

Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi mganga mfawidhi kituo cha afya kinaga Bi. Maria Chaeka alisema, kukamilika kwa kituo hiki kunakwwenda kuwanufaisha wananchi 22,243 wa kata ya kinaga na vijiji jirani ambapo kituo kinajumuisha majengo ya wangonjwa wa nje (OPD), wodi ya kujifungulia akina mama wajawazito, upasuaji, maabara, kichomea taka, kitengo maalumu cha VVU, kifua kikuu pamoja na kkiniki ya baba, mama na mtoto.


HABARI PICHA



Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa