Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd amewaahidi wananchi wa Wilaya ya Kishapu kukamilika mradi wa maji ya Ziwa Viktoria.
Akizungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Somagedi, alipotembelea Wilayani humo leo tarehe 22 Agosti, 2019, Mhe. Balozi Seif amesema kuwa, atalisimamia ombi la wananchi wa Kishapu kwa Waziri Mkuu la fedha za kukamilisha mradi wa usambazaji maji ya Ziwa Viktoria kupitia mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Suleiman Nchambi.
"Maji ni uhai, kila mtu ana haki ya kupata maji safi na salama, kwa ajili ya matumizi yake na familia yake" amesema Balozi Seif.
Akitoa ombi hilo kwa Mhe. Balozi, Mhe. Nchambi amemueleza kuwa, tayari tathmini na michoro ya usambazi wa maji ilishakamilika kinachohitajika ni fedha za kutekeleza mradi huo ili wananchi waweze kupata maji ya ziwa Viktoria.
Mhe. Balozi ameendelea na ziara yake Mkoani Shinyanga kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi akiwa ni mlezi wa Chama hicho Mkoani hapa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa