Wanaume wametakiwa kuendelea kutoa fursa kwa wanawake kutafuta, kusimamia na kubuni vyanzo vya mapato kwa ajili ya familia kwani pamoja na jukumu walilonalo wanawake la kutunza familia wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha na kukuza uchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema hayo mapema jana wakati akizungumza na wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ibadakuli, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mhe. Telack amesema kuwa, mfume dume unawanyima wanawake kufanya shughuli za kuzalisha hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.
Mhe. Telack pia amewataka Maafisa maendeleo ya jamii kuendelea kuwawezesha wanawake hasa vikundi vya ujasiriamali vinavyojishughulisha na kuzalisha bidhaa mbalimbali Mkoani hapa.
Aidha, amezitaka taasisi za fedha hususani mabenki kutoa elimu ya mikopo kwa wanawake wa Shinyanga na kuwaeleza ukweli kuhusu riba na namna ya kurudisha fedha wanazokopa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa