Na. Paul Kasembo, Shinyanga DC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka watalaam Mkoani Shinyanga kubadilika katika utendaji kazi wao na kutimizamwajibu wao kila mmoja kulingana na taaluma yake katika eneo lake badala ya kusubiria kuanza kusimamiwa, huku akimpongeza Lucia Mahena ambaye ni Mganga wa Kituo cha Afya Salawe kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa utendaji kazi mzuri anaoendelea nao.
Akiwa Salawe RC Macha amepata nafasi ya kuzungumza na wagonjwa ambao walikuwa hapa ambapo alitaka kujuwa kama wanahudumiwa vizuri, lugha zinazotumika wakati wakisubiri na wakati wakipata huduma kutoka kwa watoa huduma na kama wanapata dawa kadiri ya mahiaji yao ambapo wote kwa nyakati tofauti wamesema wanaridhishwa sana na ndiyo msingi wa RC Macha kumpongeza Daktari Lucia.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 17 Mei, 2024 wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo ameanza na Kituo cha Afya Salawe kilichopatiwa zaidi ya Tzs. Bil. 1 kwa ajili upanuzi wa jengo la Wagonjwa wa nje, Maabara, Mochwari, Kichomea taka, Mama na mtoto, jengo la upasuaji pamoja na wodi ambapo mpaka sasa majengo yote yapo hatua ya umaliziaji.
Pamoja na maelekezo mengine, RC Macha ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuweka vipaumbele katika ujenzi wake huku akipendekeza kuanza na jengo la wagonjwa wa nje pamoja na maabara ili kukabiliana na changamoto zilizopo hivi sasa katika Kituo hiki.
"Niwatake wataalam wote mbadilike katika utendaji kazi wenu wa kila siku, acheni kufanya kazi kwa mazoe, kuweni wabunifu, msiwe timizeni wajibu wenu, toeni ushauri wa kitaalam hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na mshirikiane," amsesema RC Macha.
Aidha amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jukius Mtatiro (Wakili) kukutana na wataaalm wote, mafundi na kamati zilizohusika ili kuona namna ya kuedelea na umaliziaji wa upanuzi wa Kituo hiki cha Salawe ambacho inatajwa kuwa kukamilika kwake kunakuja kuondoa adha ya upatikanaji wa baadhi ya huduma muhimu ambazo nyingine wanalazimika kuzifuata kwa zaidi ya KM 100.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa