• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

WATUMISHI WA KITUO CHA HUDUMA JUMUISHI KISHAPU, TUNZENI SIRI ZA MANUSURA NA WAHANGA WA UKATILI WA KIJINSIA - RC MACHA

Posted on: December 16th, 2024

Na. Paul Kasembo, KISHAPU.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka watumishi wa Kituo cha Huduma Jumuishi (One Stop Centre) kilichopo hapa Kishapu kutunza siri za manusura na wahanga wa ukatili wa kijinsia wanaokuja kutoa taarifa na kupatiwa huduma katika kituo hiki huku akitoa wito kwa wananchi wa Kishapu kukitumia vema na kikamilifu kwani lengo ni kutokomeza kabisa vitendo hivi visivyofaa.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 16 Desemba, 2024 wakati akizindua kituo hiki ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa Nchi ya Finland kupitia Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi Duniani (UNFPA) ambapo pamoja na kazi nyingine lakini kituo kitatoa huduma kamili za matibabu, kisheria na ushauri wa kisaikolojia kwa manusura na wahanga wa ukatili wa kijinsia na watoto wao katika sehemu moja. Huduma hizi zinaweza pia kupatikana kupitia mifumo rasmi au isiyo rasmi.

"Niwatake ninyi watumishi wa kituo hiki kuhakikisha kuwa mnatunza siri zote za manusura na wahanga wa vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia wanaokuja hapa kupatiwa huduma zenu, na hili agizo ni kukazia sehemu ya viapo na maadili yenu ya kitaaluma," amesema RC Macha.

Kwa upande wake Mark Bryan Schreiner ambaye ni Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Tanzania amesema kuwa Shirika lao litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha kuwa kunatokomezwa kabisa kwa mambo yote yanayohusu ukatili wa kijinsia na kuyalinda makundi maalum yakiwemo ya wanawake na watoto katika Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla. 

Aidha Mr Juhana Lehtinen ambaye ni Mkuu wa Ushirikiano Ubalozi wa Finland Tanzania amempongeza RC Macha kwa utendaji kazi wake huku akiishukuru zaidi Serikali ya Tanzania kwa kuendelea na mikakati ya utokomezaji wa ukatili wa kijinsia kwa wananchi wake na kupongeza kwa kazi nzuri inayofanywa na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga (SHIVYWATA) kwa kuendelea kuwaunganisha walengwa wote.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAPITIO YA ROBO MWAKA KWA KIPINDI CHA OKT - DES 2024 CHA (PJT MMMAM) CHAFANYIKA MKOANI SHINYANGA.

    February 28, 2025
  • RCC SHINYANGA YARIDHIA MAPENDEKEZO NANE (8) YA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

    February 27, 2025
  • KUKAMILISHWA KWA MIRADI YA BARABARA KUTAPUNGUZA KERO KWA WANANCHI – RC MACHA

    February 26, 2025
  • WALIMU, TOENI ELIMU INAYOENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA -RC MACHA

    February 24, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa