Na. Shinyanga RS.
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeendesha mafunzo ya kutumia mfumo mpya utakaotumika kupima utendaji kazi kwa watumishi wa umma pamoja na taasisi zake.
Mafunzo haya yaliyofunguliwa na Mwl. Dafroza Ndalichako ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambaye alimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo yanahusisha Taasisi na Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga
Serikali imekusudia kuondokana kabisa na mfumo wa awali uliokuwa unatumika kupima utendaji kazi kwa watumishi (OPRAS) na kuanza kutumia PEPMIS na PIPMIS sambamba na mfumo mpya wa kufanya tathimini ya Rasilimali Watu ofisini HR - ASSESMENT, ambapo utasaidia kutambua idadi halisi ya watumishi katika ofisi.
Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu Mkoa wa Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa