Watumishi wa Umma wametakiwa kutoepuka malalamiko yanayoletwa na wananchi kwenye Ofisi za Umma kwani yanasaidia kupata mrejesho na kujua mifumo na taratibu zilizopo kama hazipo sahihi na kufanya marekebisho ili kupata ufanisi.
Mratibu wa Utawala wa Ofisi ya Rais Bw. Francis Manyira ametoa wito huo mapema leo tarehe 08/04/2019 wakati akizungumza na watumishi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga na Taasisi za Umma zilizopo Mkoani hapa
"Malalamiko yanasaidia kupata mrejesho unaotusaidia kupata ufanisi kwa kutafuta mbinu za kutatua changamoto" amesema Bw. Manyira.
Katika kikao hicho pia watumishi wa Umma wametakiwa kujiwekea mazingira ya nidhamu kwa kujidhibiti na kujisimamia wenyewe kabla ngazi nyingine hazijawatathimini.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa