Watumishi wa Serikali Mkoani Shinyanga wameonywa tabia ya ulevi wakati wa saa za kazi pamoja na utoro bila sababu za msingi.
Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack jana wakati akizindua baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga litakalodumu kwa miaka mitatu kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Telack amesema kuna baadhi ya watumishi wana tabia ya kutoka kazini mida ya kazi na kutumia pombe hivyo kushindwa kutoa huduma kwa wananchi.
Amesema ulevi kazini ni kosa la kufukuzwa kazi hivyo, watumishi wanapaswa kufahamu hilo na kamwe hatawatetea.
Pia amesema hatataka kuona watumishi watoro na wazembe kazini. Watumishi wafanye yale walioelekezwa na mwajiri.
Aidha, Telack amewataka wajumbe wa baraza hilo kuitendea haki nafasi waliyopewa ya kuwakilisha watumishi wenzao kwa kuzungumza kuhusu changamoto zinazowakabili badala ya kuhudhuria tu kwenye vikao bila tija.
Naye Katibu Tawala Mkoa Bw. Albert Msovela amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa, Baraza hilo litafanya kazi kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu kwa muda wote wa uhai wake.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa