Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewataka wazazi kuhakikisha kuwa watoto walioandikishwa kuanza shule kuanzia kiwango cha elimu ya msingi pamoja na Sekondari wanamaliza elimu yao.
Amesema sheria iko wazi kuwa kila mzazi anapomuandikisha mtoto ahakikishe anamaliza elimu yake, mtoto akitoroka katikati hatafutwi mtoto isipokuwa mzazi.
Mhe. Telack ameyasema hayo katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli za kilimo na elimu Wilayani Kishapu, ziara atakayoifanya katika Halmashauri zote Mkoani hapa.
Amesema utoro wa aina yoyote hautaruhusiwa hivyo wataalamu watoe elimu kwa wazazi na kupita katika shule zote kuhakikisha watoto walioandikishwa wameripoti na apate taarifa ya taratibu za ufundishaji.
“kuanzia kesho wakaguzi wa elimu na maafisa elimu wapite mashuleni kukagua wanafunzi wote walioandikishwa, wote wanaoanza na wanaoendelea” ameagiza mhe. RC Telack.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa