Wazee, Viongozi wa Dini na Machifu Mkoa wa Shinyanga wamemshukuru sana Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea maendeleo ya kweli na ya haraka zaidi mkoani shinyanga. Haya yamebainishwa leo tarehe 24 Januari kwenye mkutano wa makundi hayo na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Katika mkutano huu, wazee kwa kauli moja wamesema wanamuunga mkono Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba wataendelea kushirikiana nae wakati wote na wala asiwe na shaka yoyote kuhusu Mkoa wa Shinyanga.
Kando na hayo, mkutano pia umejadilia suala ya mmomonyoko wa maadili kwa vijana ambapo hivi sasa wamefikia hatua ya kutumia madawa ya kulevya, ulevi na ukahaba wa hadharani jambo ambalo limepelekea wazee hao kutoa azimio la kumuomba Mkuu wa Mkoa kuwakamata wale wote wanaofanya biashara ya ukahaba.
Aidha, wazee, viongozi wa dini na machifu kwa kauli moja wamesema wanaridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme na hivyo wakatoa pongezi zao kwa umoja wao.
Kwa upande wake RC Mndeme amepokea pongezi za Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan na akawaahidi kuwa atazifikisha huku akiwaeleza kuwa maelekezo na ushauri wote waliotoa ameupokea na uataufanyia kazi ukiwemo wa kuhakikisha wale wate wanaofanya biashara ya uhakahaba wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya Selikali.
Picha ikimuonesha Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ndg. Ismail Makusanya akielezea jambo wakati wa mkutano
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa