#Sabasaba - 2025.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selamani Jafo, amewaomba na kuwakaribisha Watanzania wote kutoka mikoa mbalimbali kufika Jijini Dar es Salaam kushiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere, barabara ya Kilwa.
Akizungumza Julai 2, 2025 wakati wa ziara yake katika maonesho hayo, Mhe. Dkt. Jafo alisema Maonesho ya Sabasaba 2025 ni fursa muhimu kwa wananchi kutembelea, kujifunza, kununua bidhaa, kupata huduma mbalimbali za kijamii, pamoja na kujionea ubunifu wa bidhaa na huduma kutoka kwa washiriki wa ndani na nje ya nchi.
"Ni wakati muafaka sasa kwa Watanzania kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kuja kujionea fursa zinazopatikana kupitia Maonesho haya. Kuna bidhaa, huduma, na maarifa mengi ya kujifunza pamoja na kujenga mitandao ya kibiashara," alisema Mhe. Jafo.
Aidha, amesisitiza kuwa Maonesho ya mwaka huu yanatoa taswira halisi ya maendeleo ya viwanda, biashara ndogo na za kati nchini, pamoja na jitihada za Serikali katika kukuza uchumi wa viwanda kupitia ushiriki wa wadau mbalimbali wa sekta binafsi na umma.
Maonesho ya Sabasaba ni jukwaa muhimu la biashara na uwekezaji, yanayowakutanisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi, na hufanyika kila mwaka kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kukuza bidhaa za Kitanzania katika soko la kimataifa ambapo Mkoa wa Shinyanga unashiriki kikamilifu ukiwa na Mabanda 8.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa