Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea na kuziona nyumba 10 za makazi ya Polisi zilizopo Mtaa wa Kambarage, Manispaa ya Shinyanga jana katika ziara yake ya siku moja Mkoani hapa jana tarehe 09/08/2019.
Mhe. Majaliwa amekabidhi funguo kwa askari 10 watakaoanza kuishi kwenye nyumba hizo zilizogharimu jumla sh.225 milioni na kufunguliwa na IGP Said Sirro hivi karibuni.
Akikabidhi funguo kwa askari hao, Majaliwa amewataka wazitunze kama nyumba zao na wasiwe na dhana kuwa ni nyumba za Umma.
“Jukumu lenu sasa ni kuzitunza, ninaposema kuzitunza nina maana kuna baadhi ya watu tumewaona wamepewa dhamana ya kupewa nyumba, wanashindwa kutunza kwa sababau tu ni mali ya Umma” amesema Majaliwa.
“Tunarajia ukiwa mtumishi nyumba hii utaitunza kama ya kwako”
Aidha, Mhe. Majaliwa amewahakikishia wananchi kuwa, ujenzi wa makazi ya polisi ni kazi endelevu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa