• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

YEYOTE ATAKAYEKWAMISHA KAMPENI YA UGAWAJI VYANDARUA KUCHUKULIWA HATUA– RC MACHA.

Posted on: December 12th, 2024

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewatahadharisha wananchi wa Shinyanga kuwa yeyote atakayekwamisha kampeni ya ugawaji wa vyandarua vya bure vinayolenga kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Malaria atakuchukuliwa hatua za kisheria.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 12 Desemba, 2024 wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Uhamasishaji na Ugawaji wa Vyandarua kwenye kaya bila malipo kwa Mkoa wa Shinyanga, huku akisisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -TAMISEMI pamoja na wadau (Bohari ya dawa - wasambazaji wa vyandarua na Mfuko wa Dunia unaoshughulikia Afya (Global Fund) imeandaa kampeni ya Kitaifa ya ugawaji wa vyandarua katika ngazi ya kaya ikiwa ni moja ya mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

“Ninatoa tahadhari kwa wanashinyanga kuwa yeyote atakayethubutu kujaribu kukwamisha kampeni hii ya ugawaji wa vyandarua vya bure ambavyo vinalenga kudhibiti kusambaaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria atakuchukuliwa hatua kali za kisheria kwani Serikali inafanya jitihada kubwa ili kuzuia ugonjwa huu” amesema RC Macha.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni amesema kupitia kampeni hii ya ugawaji vyandarua bure inayoambatana na utoaji wa mafunzo kwa watendaji wa afya inaenda kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa matumizi ya vyandarua majumbani kwani lengo ni kuzuia maambukizi na kutokomeza Malaria.

Naye Afisa Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria kutoka Wizara ya Afya ndg. Wilfred Mwafungu ameomba ushirikiano wa pamoja kuhakikisha Kaya zote kwenye Halmashauri zote 6 za Mkoa wa Shinyanga zinafikiwa na wananchi wanapata vyandarua ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

Serikali kupitia Wizara ya Afya inafanya jitihada kubwa kuhakikisha inapiga vita maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwani ina mpango wa kuleta vyandarua zaidi ya Milioni 1 ambapo asilimia 70 ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga watapokea vyandarua bure na hivyo kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAPITIO YA ROBO MWAKA KWA KIPINDI CHA OKT - DES 2024 CHA (PJT MMMAM) CHAFANYIKA MKOANI SHINYANGA.

    February 28, 2025
  • RCC SHINYANGA YARIDHIA MAPENDEKEZO NANE (8) YA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

    February 27, 2025
  • KUKAMILISHWA KWA MIRADI YA BARABARA KUTAPUNGUZA KERO KWA WANANCHI – RC MACHA

    February 26, 2025
  • WALIMU, TOENI ELIMU INAYOENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA -RC MACHA

    February 24, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa