Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ulianza kutekelezwa tarehe 28 Machi, 2014 na ulitegemea kukamilika tarehe 28 Novemba, 2014 kwa gharama ya sh.900,799,180 pamoja na VAT. Mkandarasi wa Mradi huu ni Kampuni ya M/S STANCE TECHNIC AND CIVIL ENGINEERING LTD ya Arusha na Mhandisi mshauri ni Wakala wa Majengo (TBA) kwa gharama ya sh.94,044,000/=. Mkandarasi aliongezewa muda na kutakiwa kukamilisha kazi tarehe 30 Aprili, 2016 kwa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;-
FEDHA ZILIVYOTUMIKA.
Baadhi ya kazi za kukamilisha jengo hilo bado kufanyika kama vile kujenga mfumo wa maji safi na maji taka, kuweka masinki ya kunawia mikono, masinki ya vyooni, kujenga kichomea taka na kujenga kibanda cha walinzi.
CHANGAMOTO
Mradi kutokamilika kwa wakati kwa Mkandarasi kushindwa kutekeleza ujenzi huo na kukabidhi.
CHANGAMOTO ZILIVYOSHUGHULIKIWA
Kwa kuwa Mkandarasi ameshindwa kumaliza kazi kwa muda wa mkataba, Mwajiri anakusudia kumsimamisha kazi Mkandarasi M/S STANCE TECHNIC AND CIVIL ENGINEERING LTD wa Arusha, maelekezo ya Mkandarasi Mshauri (TBA) yanasubiriwa ili hatua za kumsimamisha kazi Mkandarasi ziweze kuchukuliwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa