Ujenzi wa Jengo la Damu salama lilijengwa katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Manispaa ya Shinyanga. Jengo hilo lilianza kujengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilianza tarehe 27 Juni, 2016 na kukamilika tarehe 07 Agosti, 2016 kwa gharama ya fedha za Kitanzania sh.33,435,000/= (Thelathini na tatu millioni, laki nne thelathini na tano elfu). Awamu ya pili ilianza tarehe 01 Novemba, 2016 na kukamilika tarehe 26 Disemba, 2016 kwa gharama ya sh.46,224,400/= (Arobaini na sita millioni, laki mbili na ishirini na nne na mia nne). Jumla ya gharama za ukamilishaji wa jengo hilo ni sh.79,659,400. Jengo hilo limejengwa na kampuni ya M/S FAU CONSTRUCTION CO.LTD wa S.L.P. 1289, SHINYANGA.
Mpaka sasa jengo la Damu Salama linatoa huduma zilizokusudiwa za kukusanya Damu ijulikanayo kama (Benki ya Damu) kwa ajili ya matumizi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa