Mpango wa kuinua ubora wa elimu Tanzania unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo laUingereza, unasaidia kuboresha elimu kwenye zaidi ya Shule za msingi 5000 za Serikali ya Tanzania.
EQUIP-Tanzania inasaidia Serikali ya Tanzania kuongeza ubora wa matokeo ya ujifunzaji kwenye shule za msingi, hasa kwa wasichana. Inajikita kwenye mfumo maalumu wa uboreshaji unaozingatia gharama ambazo zinaleta mabadiliko kwa njia ambazo zinaweza kutumiwa nchi nzima. Utekelezaji wa mpango ulianza mwaka 2014 kwa Mikoa mitano na baadae mikoa saba (Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Lindi, Mara, Dodoma,Tabora). Baadaye mwaka 2017, Mikoa mingine miwili zaidi ikaongezwa (Singida, and Katavi), ambapo kwa pamoja inaleta jumla ya shule zaidi ya 5000 na wanafunzi milioni 2.3.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa