BARAZA la biashara mkoa wa shinyanga liliofanyika tarehe 19 Desemba, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa limelipongeza Jukwaa la wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga (SBF) ambalo mratibu wake ni Ndg. Mussa Ngangalas kwa kufanya vema katika maonesho yake ya 2023 lilifanyika katika viwanja vya Karena Hotel iliyopo Manispaa ya Shinyanga na kudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali wa ndani na nje ya mkoa wa shinyanga.
Akitoa pongezi hizi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alisema kuwa, Jukwaa la Biashara Shinyanga limefanya kitu kizuri sana katika kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa kada mbalimbali yaani wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa ili kutoa nafasi ya kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta ya biashara kwa mkoa wa Shinyanga kwa mwanzo huu Baraza la Biashara Mkoa wa Shinyanga linawapongeza sana.
"Kwa niaba ya Baraza la Biashara Mkoa wa Shinyanga, tunawapongeza sana Jukwaa la Biasahara Shinyanga (SBF) kupitia Mratibu wa SBF Ndugu Mussa Ngangalas kwa kuweza kuandaa, kusimamja na kutekeleza maonesho yenu yaliyolenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa kada zote ambapo wamepata fursa ya kufahamiana na kuongeza mtandao wa biashara zao, hongereni sana SBF", alisema RC Mndeme.
Baraza pia lilipata bahati ya kuhudhuriwa na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Bi. Anna Makinda akiwa na wataalam wake, ambapo pamoja na pongezi kwa baraza kwa kazi nzuri wanazofanya lakini nao walipata nafasi ya kuwasilisha taarifa mbalimbali za ofisi za takwimu ikiwemo matokeo ya sensa ya watu na makazi ya 2022.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga wakatiwa kikao
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akielezea jambo wakati wa kikao
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa