Majukumu ya Idara ya Huduma za Maji
•Kutathimini, kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa sera za sekta ya maji katika Mkoa
•Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye sekta ya Maji
•Kuwasiliana au kuwa daraja kuunganisha baina ya Mamlaka zinazohusika kwenye Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya masuala yanayohusu sekta ya Maji.
•Kuendeleza na kuboresha hali ya huduma za maji na usafi wa mazingira katika Mkoa.
•Kuwezesha, kuratibu, Kusimamia, na kuthibiti sekta binafsi zinazotoa huduma za Maji katika Mkoa.
•Kuwezesha na kuratibu timu ya huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika Mkoa.
•Kuzisaidia na Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kutambua na kuimarisha vyombo huru vya watumiaji maji.
•Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa Miongozo ya utekelezaji na ukarabati wa miradi ya Maji
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa