BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) limeanza uhamasishaji na mafunzo ya urasimishaji biashara na fursa za ununuzi wa Umma kwa wafanyabiashara wadogo nawa kati katika Mikoa mbalimbali nchini ambapo Shinyanga ni moja ya Mkoa uliopata fursa ya mafunzo haya.
Akizungumza kwa niaba ya Timu ya wawezeshaji Bi. Susan Masalla kutoka NEEC amesema kuwa pamoja na kufanya uhamasishaji na mafunzo haya, lakini pia washiriki watapata nafasi nzuri ya kujifunza namna nzuri ya kufanya Ununuzi wa Umma, usimamizi wa biashara rasmi, taratibu za kukamilisha urasimishaji na maana halisi ya urasimishaji wa biashara yenyewe.
Mafunzo haya ya siku tatu kuanzia tarehe 20 - 22 Desemba, 2024 kwa upande NEEC yanawakilishwa na Susan Masalla, Barry Yongolo na Jozaka Bukuku, PPRA inawakilishwa na mkufunzi ndg. Lusekelo Kamwena huku ndg. Chrisantus Kitundu yeye ni Mwalimu wa Uanzishwaji na Uendelezaji Biashara, wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ni Mha. Dotto Maligisa na Rose Tungu.
Na makundi nufaika katika mafunzo haya kwa napa mkoani Shinyanga ni pamoja na Jukwaa la Wanawake Kiuchumi, Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Chama Cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), Wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 pamoja na Vikundi vya Wajasiliamali.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa