Na Shinyanga RS.
Katika kuboresha wajibu wa wamiliki wa leseni za madini kwa jamii nchini (CSR) Mgodi wa Barick bulyanhulu kwa kushirikiana na Tume ya madini Mkao mkuu Wamefanya mafunzo ya kanuni mpya za CSR kwa Viongozi wa Halmashauri ya Msalala kwaajili ya kurahisisha Uaandaji na Utekelezaji wa miradi Itakanayo na CSR.
Akieleza Umuhimu wa Mfunzo hayo Mhandisi Migodi kutoka Tume ya Madini Mako makuu MACKENZIE MABULA Amesema Awali kulikuwa na Sheria pekee zilizokuwa zinatumika ambapo kulikuwa nachangamoto ya kuzielewa sharia zote hivyo ujio wa kanuni hizi zitawarahisishia wasimamizi na watekelezaji wa miradi hiyo itokanayo na CSR.
“Niseme tu ujio wa kanuni hizi zitawasaidia sana katika uandaaji na utekelezaji wa miradi hii kuchambua sharia moja baada ya nyingine kulikuwa nachangamoto zake lakini sasa serikali yetu imeliona hilo sasa tutatumia kanuni niwaombe kwa pamoja mgodi na halmashauri mkatekeleze ipasavyo miradi hiyo” –Mabula alisema
Kwa Upande wake Meneja wa wa Mazingira na Mahusiano ya Mgodi wa Bulyanhulu AGAPITI PAUL Ameiomba halmshauri hiyo kuendelea kushirikiana na mgodi kwa kukamilisha miradi kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na uwekezaji uliofanywa na mgodi huo wa Bulyanhulu .
“Tujitahidi kumaliza kwa wakati miradi hii kwani lengo la mgodi na serikali ni kuona wananchi wananufaika na wawekezaji nchini hasa sisi wa madini ambao tumewekeza katika halmashauri yenu” –PAUL alisema
Akifunga mafunzo hayo kwa upande wa Halmshauri ya Msalala Mkurugenzi Mtendaji Khamis katimba Ameupongeza mgodi wa Barick bulyanhulu kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatawasaidia waatalamu wake kutekeleza kwa ufanisi Miradi hiyo itakayotolewa na Mgodi huo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa