Na. Shinyanga RS.
MRAJIS Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi Hilda Boniphace amefungua Mafunzo ya Mfumo Mpya wa Usambazaji na Uuzaji wa Mbolea za Ruzuku 2023/2024 kupitia Vyama vya Ushirika Mkoani Shinyanga na kuwataka viongozi kuwa waaminifu ns wazalendo wakati wa kusimamia mfumo huo ili uweze kuleta tija kama ilivyokusudiwa.
Hilda amesema maelekezo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa mbolea za ruzuku zinawafikia wakulima wote ambao ndiyo hasa walengwa na kwa urahisi zaidi huku akivitaka vyama kwenda kujipanga kwa ajili ya kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wakati wa zoezi hili.
Aidha, Bi Hilda ameishukuru sana Serikali ya awamu ya sita inauoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara kwa kuipatia dhamana hii kubwa vyama vya ushirika ili kuwezeaha huduma kuwafikia wakulima wote na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali.
Uwepo wa Mafunzo haya ambayo yamehusisha vyama vikuu na wanachama wa TANCCOOP kutoka Mikoa ya Simiyu, Geita, Mwanza, Singida, Mara ,Tabora na Shinyanga ambao makao makuu yake ni hapa Mkoani Shinyanga unatajwa kuwa mwarobaini wa urasimu katika kuwapatia huduma wakulima ambao ndiyo wadau muhimu wa mfumo huu.
Picha ikionesha baadhi ya washiriki wa mafunzo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa