• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

BILIONI 846 ZABORESHA SHUGHULI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII SHINYANGA - RC MACHA

Posted on: October 9th, 2024

Na.Paul Kasembo, TINDE.

MKUU  wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Anamringi Macha ameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha fedha takribani Bilioni 846 ndani ya miaka 3 kwa ajiri ya kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii mkoani Shinyanga ambapo hivi sasa takribani vijiji vyote 506 na mitaa yote imefikiwa kwa miradi tofauti tofauri ikiwemo ya afya, elimu, miundombinu, maji, umeme uwezeshaji wananchi kiuchumi nk.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 9 Oktoba 2024 akiwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu CCM Balozi. Dkt. Emmanuel Nchinbi kwenye Kata ya Tinde iliyopo Wilaya ya Shinyanga huku akimpongeza sana Dkt. Nchimbi kwa kazi nzuri anazozifanya.

“Naishukuru sana Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kiasi cha fedha takribani Bil. 846 ndani ya miaka hii 3 kwa ajiri ya kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii, nasi hatuna budi kuendelea kuhakikisha fedha hizi zinatumika kama zilivyopangwa kwa maendeleo ya wananchi wa Mkoa wetu,” amesema RC Macha.

Akizungumza na Wananchi wa Kata Balozi Dkt. Nchimbi amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Macha kuendelea kutatua changamoto na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kata ya Tinde na Mkoa kwa ujumla ili kuhakikisha wanaenda sambamba na kasi ya ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo.

Dkt. Nchimbi akiwa ameambata na Sekretarieti ya CCM Taifa atafanya ziara ya siku 3 katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kahama Manispaa na mwisho Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kuimarisha Chama cha Mapinduzi, kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama pamoja na kupokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRADI WA TABLET KWA SHULE ZA MSINGI WATAMBULISHWA NGAZI YA MKOA WA SHINYANGA NA WILAYA

    June 03, 2025
  • SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA, WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

    June 02, 2025
  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa