Na. Shinyanga RS
MKUU wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude leo tarehe 6 Machi, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ameshuhudia utiaji saini kati ya Mgodi wa Williamson Diamond Limited na Halmashauri ya Kishapu ambapo jumla ya Tzs. Bilioni moja imetolewa na Mgodi kwa ajilia Mrejesho kwa Jamii utokanao na Mapato Ghafi kwa mwaka 2024/2025.
Akizungumza wakati utiaji saini huu, Mhe. Mkude ameutaka uongozi wa mgodi kuimarisha uhusiano wake na wanajamii wanaozunguuka mgodi sanjari na kuwashirikisha kwa kila kitu ikiwemo kujuwa mipango yao dhidi wananchi jambo litakalopelekea wao kuwa sehemu ya umiliki pamoja kuimarisha uhusiano na mawasiliano kati yao na Halmashauri ya Kishapu kabla, wakati na baada ya kuanza kutekeleza miradi kwa jamii ili kuepuka kujirudia rudia kwa miradi hiyo.
"Niwatake Uongozi wa Mgodi kuimarisha uhusiano kati yenu na Jamii pamoja na Halmashauri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, jambo ambalo litaifanya jamii kuwa sehemu ya umiliki, kuwa sehemu ya ulinzi wa mali na mgodi sanjari na kuepuka mgongano wa miradi iliyopendekezwa na Halmashauri na ile ya Mgodi", amesema Mhe. Mkude.
Akizungumza kwa niaba ya Mgodi Ndg. Bernald Mihayo ambaye ni Afisa Uhusiano amesema kuwa, urejeshwaji wa fedha hizi ambazo zinatokana na gawiwo la 0.7% ya Mapato Ghafi ni utekelezaji wa takwa la kisheria, huku akiwaomba wananchi kuwa sehemu ya umiliki wa Mgodi huu ikiwa ji pamoja na kuzuia hujuma jambo ambalo lawezapelekea kushuka kwa uzalishaji na mrabaha pia ambao wao ndiyo wanufaika zaidi.
Utiaji saini huu wa Hati ya Makubaliano (MoU) unatajwa kuwanufaisha wananchi wa Wilaya ya Kishapu, maalumu wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Williamson Diamond Limited ambapo Tzs. Bilioni 1 zimetolewa kwa mchanganuo wa Milioni 600 kutekeleza miradi ya kimkakati na Milioni 400 itarejeshwa katika vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa