Repost from @nirc_tz
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika (MB) imeridhishwa na utekelezaji wa miradi inayofanywa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), ikiwemo ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Nyida uliopo Halmashauri ya Manispaa mkoani Shinyanga.
Kamati hiyo imetembelea mradi huu Machi 13, 2025 ili kujionea utekelezaji wa mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Nyida unaogharimu Tzs. Bilioni 13.6 utakaonufaisha eneo la Umwagiliaji la hekta 800 kwa Nyida na hekta 1,500 kwa Lyamalagwa na zaidi ya wakulima 4,5000 watanufaika, na hivyo kuakisi kinachofanywa na Tume kinaendana na thamani ya fedha inayowekezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miradi ya umwagiliaji nchini.
Akizungumza katika ziara fupi ya kukagua miradi hiyo mkoani Shinyanga, Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Deodatus Mwanyika, amesema kamati inaridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba thamani ya fedha inaonekana, huku akiongeza kuwa anaamini malipo yaliyobaki ya kiasi cha Tzs Bilioni 5.6 ili kukamilisha mradi huo unaogharimu Tzs. Bilioni Sh13. 6 yatafanyika kwa wakati ili wananchi waone na kufurahia matunda yake.
“Kamati inaridhishwa kwa kiasi kikubwa na utekelezaji w mradi huu hata kwa macho ukiangalia ujenzi wa ofisi, bwawa na miundombinu mingine inaridhisha na Tzs. Bilioni 8 zilizoanza kufanyiwa uwekezaji zimetumika ipasavyo na zinaonekana, hivyo tunaamini kuwa malipo yaliyobaki kukamilisha mradi huu yatafanyika kwa wakati ili wananchi waweze kuona na kufurahia matunda ya mradi huu, " amesema Mhe. Deodatus.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, alisema mkoa unaipongeza Wizara na NIRC kwa kazi kubwa inayofanyika katika ya miradi ya Umwagiliaji kwani mara kwa mara ametembelea mradi huu na amejionea Tume inafanya mambo makubwa chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe ameahidi atafanya uwekezaji hapa kwa kujenga mashine na ghala hivyo wakulima wa mpunga watauza mchele na kunufaika zaidi kiuchumi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa