Na. Shinyanga RS.
Kuelekea Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imewajengea uwezo maafisa na wadau mbalimbali watakao toa huduma za kisheria katika maeneo yote ya Mkoa.
Akieleza mbele ya wajumbe hao, Msajili Msaidizi wa watoa huduma ya Msaada wa Kisheria ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Ndg. Tedson Ngwale amesema kuwa ujio wa Kampeni hii ya ijulikanayo Mama Samia Msaada wa Kisheria (Mama Samia Legal Aid Campaign) katika Mkoa wa Shinyanga itawasaidia sana wananchi katika kutatua kero zao sambamba na kupata haki zao kwa wakati.
"Ujio wa Kampeni hii ya Mama Samia Msaada wa Kisheria ni mwarubaini wa kero, shida na changamoto zote zinazohusu upatikanaji wa haki kwa wakati walizojuwa wakikutana nazo wananchi wa Mkoa wa Shinyanga hasa wale wasiokuwa na uwezo, makundi maalumu yakiwamo wanawake na watoto jambo ambalo awali walikuwa wakisubiria ziara za viongozi wa ngazi za juu ili watoe kero zao," alisema Ngwale.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Msaada wa Kisheria kwa Wananchi Mkoa wa Shinyanga Ndg. John Shija alisema kuwa Kampeni hii ni muhimu sana kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ili kuweza kuondoa kabisa kero ambazo zimekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya wananchi, huku akitoa rai kwa watoa huduma hiyo kuwa wasiende kutekeleza tofauti na kusudio la kampeni na kuwa sehemu ya wanaharakati.
Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria kimkoa utafanyika rasmi tarehe 11 Juni, 2023 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Christina Solomon Mndeme Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ikiwa na Kauli Mbiu "Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo"
Picha ikionesha baadhi ya wajumbe walioshiriki katika uwezesho wa masuala ya Msaada wa Kisheria katika Mkoa wa Shinyanga
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa