LAAC YAIPONGEZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA
Na. Paul Kasembo - Shinyanga RS.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya Serikali inayoakisi thamani halisi ya fedha na yenye tija kwa wananch.
Haya yamebainishwa tarehe 27 Machi, 2024 na Kamati hii ambayo imeongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Stanslaus Mabula (MB) ambapo katika ziara hii ambayo imejumuisha miradi miķubwa miwili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga pamoja na ujenzi wa Soko Kuu, huku wakitoa wito kwa Halmashauri nyingine kuja kujifundisha hapa namna bora ya uendeshaji wa miradi kama inavyofanya Shinyanga Manispaa.
"Tunawapongeza sana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa utekelezaji bora wa miradi ya maendeleo yenye kuakisi thamani ya fedha na yenye tija kwa wananchi, na kwa msingi huu tuzitake Halmashauri nyingine kuja kujifundisha hapa Manispaa ya Shinyanga namna bora ya kutekeleza miradi ya maendeleo," amesema Mhe. Mabula.
Kukamikika kwa shule ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga kunatajwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia wanafunzi ambapo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 880 hadi 1200.
Na kwa upande wa Soko Kuu, kunatajwa kuja kuongeza mzunguko wa biashara, fedha na kuongeza pato la wakazi wa Shinyanga, kuongeza na kuboresha mazingira, kuongeza mvuto na muonekano wa mji ambapo kwa sasa hatua inayofuata ni ufungaji umeme katika mabanda yote 52 ya chini na kukamilisha mabanda 54 yote ya juu ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024 ili yatumike yote.
HABARI PICHA
Prof. Siza Tumbo (mwenye suluali nyeusi) akiongoza ujumbe wa Kamati ya LAAC kukagua miundombinu ya Shule ya Sekondari Shinyanga Wasichana.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa