Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KIONGOZI wa ubunifu na msimamizi wa chapa ya jambo group, ndg. Nickson George amesema kuwa MAKAMPUNI ya mzawa "jambo Group" yameamua kutoa shukrani kwa wateja na watumiaji wa bidhaa zake za jambo kwa kuzindua Kampeni ya Selebretika Kijamukaya ambapo inazalisha bidhaa zake zenye chapa maalumu kwa ajili ya msimu wa sikukuu ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini hadhi, umuhimu na sapoti ya wateja wake waliounga mkono bidhaa zao kwa mwaka mzima.
Nickson amesema haya tarehe 21 Desemba, 2024 kwamba kando na shukrani kwa wateja wake, pia uwepo wa kampeni hii ni kuona watu wote wanasheherekea sikukuu zilizopo mbele yetu wakiwa na furaha, amani na upendo pamoja na familia zao.
"Wanafamilia wa Makampuni ya Mzawa JAMBO GROUP tunayo furaha kubwa kuanza kutoa shukrani zetu kwa watumiaji na wateja wetu wote kwa ujumla wao kwa kutuunga mkono mwaka mzima, na kipekee katika hili tumetengeneza bidhaa zetu chapa mpya ya "Selebretika Kijamukaya" ikienda sanjali na Kampeni yenye lengo la kutambua na tuthamini sapoti ya wateja wetu," amesema Nickson.
Makampuni ya jambo Group yanajishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali yanejichukulia umaarufu mkubwa kupitia bidhaa zake bora na pendwa zenye uhalisia mkubwa kwa watu wa rika zote zikiwemo za vinywaji baridi kama vile juisi, maji, Jambo Malta Lemon, Jambo Apple, Jambo Embe, Jambo Energy, Jambo Malta Pineapple, Jambo Lemon, Jambo Vito, Jambo Orange, Jambo Drinking Water na vingine vingi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa