Na. Shinyanga RS.
Muwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahim M. Makana amezielekeza shule na vyuo vyote Mkoa wa Shinyanga kuanzisha Klabu za Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mwanafunzi wenye maadili mema na kuongeza ufaulu katika masomo yao
Makana ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Menejimenti ya Ufuatiliaji na Ukaguzi Mkoa wa Shinyanga aliyemuwakilisha Katibu Tawala Mkoa Pro. Siza Tumbo pamoja na mambo mengine aliwaeleza washiriki wa mafunzo kuwa, uwepo wa klabu hizi kunakwenda kuimarisha uwezo wa walimu katika kusimamia klabu hizi ngazi ya shule na vyuo jambo ambalo litapelekea kuwa na wanafunzi ambao ni raia wema, viongozi bora na wazalendo kwa taifa letu.
"Nazielekeza shule zote na vyuo vyote hapa mkoani shinyanga kuhakikisha zinaanzisha klabu hizi za maadili ya uongozi wa umma kwakuwa kuna uhusiano mkubwa sana kati yake na ufaulu wa masomo ya wanafunzi", alisema Makana.
Kwa Upande wake Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Ndg. Gerald Mwaitebele amesema kuanzishwa kwa klabu hizi zitasaidia kuwajengea wanafunzi kujua maadili yanayopaswa kuzingatiwa katika ujenzi wa Taifa letu pamoja na kuwa wamzalendo wa kweli.
Kwakuwa ili Taifa liweza kupata viongozi wenye maadili na kizazi chenye uadilifu, ni muhimu walimu kutumia njia vikao vya wazazi mashuleni ili kufikisha ujumbe wa mambo ya maadili kupitia klabu walizozianzisha.
Aidha, Ndg. Mwaitebele ameeleza sifa za mwalimu anayefaa kuwa mlezi katika klabu za maadili ikiwemo Mwadilifu, Mwaminifu, Muwazi,Mzalendo, Mchapakazi na anayekubalika kimaadili na wanafunzi.
Mwaitebele na timu yake ya maadili wwakiwa na waratibu wametembelea shule na vyuo mbalimbali ambazo tayari zimeanzisha klabu hizi za maadili ambapo wamesikiliza ngonjera, mashairi, maigizo na nyimbo kutoka kwa wanafunzi zikiwa na lengo la kuhamasisha na kukuza maadili ya umma na kwa watu wote.
Ndg. Gerald Mwaitebele Katibu Msaidizi OR, Sekretalieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi
Ndg. Onesmo Msalangi Afisa Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi
Mwl. Bakari Kasinyo (aliyesimama) ambaye Mratibu wa Klabu za Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa wa Shinyanga
Picha ikionesha walimu wa klabu za maadili wakiwa katika mafunzo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa