KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Ndugu Paul Makonda amezindua rasmi kitaifa wiki ya maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi akiwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Town ambapo pia alikuwa akihitimisha ziara yake ya siku mbili ndani ya Mkoa wa Shinyanga.
Makonda amesema kuwa CCM inatimiza miaka 47 ya kuzaliwa kwake ambapo kuanzia leo tarehe 28 Januari, 2024 hadi tarehe 4 Februari, 2024 ndiyo mwisho wa wiki ya maadhimisho na tarehe 5 Februari, 2024 itakuwa kilele cha sherehe.
"Napenda kutumia fursa hii kutangaza rasmi kuwa leo hapa Manispaa ya Shinyanga hapa Mkoa wa Shinyanga, nazindua rasmi Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 47 ya CCM yenye Kauli Mbiu Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu na Kazi Iendelee", alisema Makonda.
Kando na uzinduzi huu, Makonda pia amepata wasaa wa kuhutubia wananchi, kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambapo pamoja na mamb9 mengine alisisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kuwa waadilifu katika kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutumia vema lugha katika kuwajibu.
Aidha, Makonda amesema kuwa CCM haitambeba mtumishi yeyote mzembe, asiyekuwa muadilifu na asiekuwa na ambaye hatoi huduma bora kwa wananchi, CCM haitambeba mtumishi huyo, alisisitiza Makonda.
Mkutano huu unaofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Town unahitimisha ziara ya siku mbili ya ndugu Makonda katika Mkoa wa shinyanga iliyoanza tarehe 27 hadi 28 Januari, 2024 ambapo amefika, kuhutubia, kusikiliza na kutatua kero katika Manispaa ya Kahama, Kata ya Segese iliyopo Halmashauri ya Msalala, Kata ya Kakola.
Na siku ya pili alianza na wananchi waliokuwepo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kahama kisha akasimama Kata ya Kagongwa, Mwakata, Tinde na kisha hapa viwanja vya Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa