• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

MASUDI KIBETU AFUNGUA MAFUNZO YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA - KAHAMA

Posted on: October 24th, 2024

Na. Paul Kasembo, KAHAMA.

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ndg. Masudi Kibetu amefungua mafunzo ya viongozi wa Vyama vya Siasa Wilaya ya Kahama na kuwaomba kuendeleza amani, upendo na mshikamano kama ilivyo sasa hivi kwani wanapaswa kuendelea na maisha baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopo mbele yao.

Kibetu ameyasema haya leo tarehe 24 Oktoba, 2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambapo jumla ya Vyama 16 vya Siasa vimehudhuria Mafunzo ili kufahamu Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.

"Niendelee kuwaomba na kuwasisitiza tena kuwa, kama ambavyo tunavyoishi hivi sasa kwa upendo, umoja na mshikamano wetu tuendelee nao wakati na baada ya uchaguzi kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi huu," amesema Kibetu.

Awali akitoa Elimu hii kwa wajumbe, Frank Shija ambaye ni mwezeshaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kuwa, viongozi wanapaswa kuzisoma na kuzielewa vema Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo  inayotolewa na Ofisi ya Msajili ili ziweze kuwasaidia na kuwaepusha kutenda makosa ambayo yanaweza kuepukika na kwamba uzalendo, utu na hekima vikawe sehemu ya kampeni zao hata baada ya uchaguzi.

Kwa upande wao viongozi wa vyama vya siasa kwa nyakati tofauti wameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhakikisha kunakuwa na usawa kabla, wakati na baada ya uchaguzi huu kwani ofisi hiyo ndiyo mlezi wa vyama vyote huku wakisisitiza kuwa wanayo imani kubwa na Msajili wa Vyama huku wakiiomba iwe na utaratibu wa kushuka ngazi za chini kukutana na kuzungumza na viongozi hawa kama walivyofanya hivi sasa au kusubiria mpaka kutokee uchaguzi kama hivi.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania inaendelea na zoezi la utoaji wa elimu na mafunzo kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhusu Sheria zinazosimamiwa  ambapo walengwa ni viongozi wa vyama hivi vya siasa ikiwa ni kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka huu.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRADI WA TABLET KWA SHULE ZA MSINGI WATAMBULISHWA NGAZI YA MKOA WA SHINYANGA NA WILAYA

    June 03, 2025
  • SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA, WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

    June 02, 2025
  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa