Na. Paul Kasembo, SHY RS.
Mratibu wa safari ya mashabiki wa Stand United Football Club (Chama la Wana) ya Shinyanga Bi. Jackline Buhali watakaokwenda kuishangilia katika mchezo dhidi ya Geita Gold FC utakaochezwa January 12, 2025 amesema kuwa Mhandisi James Jumbe kama mdau wa michezo anauchukulia kwa uzito mkubwa mchezo huo na ndiyo sababu ameamua kuwalipia gharama za kwenda na kurudi Geita mashabiki zaidi ya 200.
Bi. Jackline ameyasema haya Januari 10, 2025 alipokuwa akizungumza na Wandishishi wa Habari mkoani Shinyanga juu ya uwepo wa ufadhiri huu kwa mashabiki na umuhimu wa mchezo huo kwa Mha. Jumbe mchezo ambao utakaofanyika mkoani Geita 12 Januari, 2025 huku donge nono la Sh, 3 Milioni likitangazwa kwa ushindi wa timu na motisha kwa ya Tzs. Laki mbili kwa kila bao litakalofungwa.
"Mhandisi Jumbe ameuchukulia kwa uzito mkubwa mchezo wa Championship kati ya Stand United FC (Chama la Wana) na Geita Gold FC utakaochezwa Januari 10, 2025 Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita na ndiyo maana ameamua kuwalipia gharama ya kwenda na kurudi mashabiki zaidi ya 200 watakaokwenda kuishangilia timu hiyo," amesema Bi. Jackline.
Hii ni sehemu ya kurejesha heshima ya Mkoa wa Shinyanga katika soka kwa kusapoti timu hii inayodhaminiwa na Makampuni ya Jambo Group sanjari na kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza Sekta michezo nchini.
Kwa uapnde wake Afisa Habari wa timu ya Stand United FC ndg. Ramadhani Zoro pamoja na shukrani nyingi kwa Mhandisi Jumbe, amesema wachezaji wote wana afya njema, ari ya kucheza na nguvu ya kutosha na kwamba mashabiki wote waendelee kuisapoti timu hiyo na watarajie matokeo ya ushindi kuelekea mchezo wao dhidi ya Geita Gold FC wakiwa ugenini.
Stand United FC ya mkoani Shinyanga inayocheza Ligi ya Championship kwa msimu wa 2024/2025 mpaka sasa imecheza jumla ya michezo 14 na kukusanya alama 29 na inatazamwa kama moja ya timu yenye kuleta matumaini ili msimu ujao Mkoa uweze kupata timu ya Ligi Kuu kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita ambapo mkoa huu ulikuwa na timu za Mwadui FC na Stand United FC.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa