MHE. CHEREHANI AONGOZA HARAMBEE
USHETU.
Zaidi ya Shilingi Milioni 50 zimekusanywa katika harambee iliyofanyika kwa ajili ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Chona iliyopo katika Kata ya Chona Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Fedha hizo zimekusanywa katika hafla ya kufungua Mwaka iliyofanyika leo ambayo imewahusisha wadau mbalimbali wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Emmanuel Cherehani, Diwani wa Kata ya Chona ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, Mkurugenzi wa Gold FM Bi. Neema Mghen pamoja na wadau wengine ambapo kiasi cha shilingi milioni 25 zimepatikana huku shilingi milioni 25 zikiahidiwa.
Akizungumza katika hafla hiyo Mbunge Cherehani ameitaka Kamati ya Shule hiyo kusimamia vyema fedha hizo ili ziweze kukamilisha ujenzi huo huku akiwakumbusha wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wao ili waweze kutimiza ndoto zao na kuzisaidia familia zao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mabala Mlolwa amesema kukamilika kwa bweni hilo kutamsaidia mtoto wa kike katika kutimiza ndoto zake, huku Mkurugenzi wa Gold FM Bi. Neema Mgheni akiwahimiza Wadau wengine wa Maendeleo kuendelea kujitoa katika sekta ya elimu.
Awali akisoma risala Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Masamaki Madaha amesema watoto wa kike wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutembea zaidi ya kilomita 10 kuifikia shule pamoja na kurubuniwa na kutumbukia kwenye vitendo vya ngono hali inachangia kukatisha masomo yao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa