Na. Shinyanga RS
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi leo tarehe 8 Novemba, 2023 amegawa vifaa mbalimbali ikiwemo Blangeti na Mahindi kwa wahanga wa mvua kubwa iliyopelekea kuezuliwa paa na baadhi kubomoka nyumba na kuathiri makazi yao kwa mvua kubwa iliyonyesha Oktoba 17, 2023 ambapo jumla ya Kaya 8 zilikosa kabisa makazi ya kuishi huku akimshukuru na kumpongeza sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali na kuwathamini sana wananchi wake.
Akikabidhi mahitaji hayo katika Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Chibe Mhe. Samizi alitanguliza pole kwa wahanga wote huku akitoa tahadhari ya kuwataka wajenge nyumba zenye uimara mara baada ya kipindi cha mvua kuisha ili kuepukana na maafa makubwa ya kukosa makazi ya kuishi wakati mwingine.
"Poleni sana ndugu zangu kwa maafa yaliyowapata, niseme tu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anawajali, anawathamini na anawatambua sana ndiyo maana leo nipo hapa kwa ajili ya kuwapatia vitu hivi ikiwemo blangeti kwa ajili ya kujikinga na baridi pamoja na mahindi ya chakula lakini pia niwatake msimu wa mvua utakapopita tuboreshe nyumba zetu na tujenge nyumba zenye uimara" amesema Mhe. Samizi.
Mhe. Samizi alisema kuwa, Mhe. Rais kama mama, mama huwa anahakikisha watoto na jamii yake inapata hifadhi na chakula wakati wote, hivyo serikali ya awamu ya sita ya Mhe Rais imewashika mkono wahanga wa mvua kwa chakula (mahindi) na mablanketi ambapo jumla ya tani 4.776 zimepokelewa huku Chibe wakipata tani 0.96 sawa na kilo 960.
Jumla ya blangeti 40 katika kaya 8 zenye watu 40 pamoja na mahindi tani moja (1) kwa jumla ya watu 40.
HABARI PICHA.
MHE. JOHARI SAMIZI KATIKA UGAWAJI WA MAHINDI NA BLANGETI KWA WAHANGA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa