• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

MKOA WA SHINYANGA UNAFAA SANA KWA UWEKEZAJI WA AINA YOYOTE - DKT. MAGEMBE

Posted on: January 24th, 2025

SHINYANGA RS.

MWENYEKITI wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Binilith  Mahenge amesema Mkoa wa Shinyanga unafaa sana kwa uwekezaji wa aina yoyote kwakuwa una kila kitu cha muhimu ikiwemo rasilimali watu, vitu, miundombinu ya Reli, barabara, uwanja wa ndege wa Kahama ambao mpaka sasa unatumika, uwanja wa ndege wa Shinyanga ambao utakamilika hivi karibu, maji na umeme wa uhakika.

Dkt. Magembe ameyasema hayo leo tarehe 23 Januari, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga ambapo akiwa ameongoza na wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wametembelea na kuona uzalishaji katika Kiwanda cha Jielong Holding (T) LTD kilichopo Manispaa ya Shinyanga na kinachozalisha Mafuta ya Pamba na Alizeti.

Pamoja na pongezi kwa uongozi wa Kiwanda, pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wakulima na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani kuongeza kasi ya uzalishaji malighafi ambazo ndiyo muhimu kwa uzalishaji na uendeshaji wa viwanda kikiwemo hiki cha Jielong Holding (T) LTD.

"Mkoa wa Shinyanga ni mahali sahihi, panafaa sana kwa uwekezaji wa aina zote ikiwemo viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na ukizingatia kuna kila kitu muhimu kwa uwekezaji kama vile barabara za uhakika, reli na ujio wa reli ya kisasa (SGR) uwanja wa ndege wa Kahama ambao unafanya kazi, uwanja wa ndege wa Shinyanga ambao upo hatua za mwisho kukamilika, umeme wa uhakika, maji na rasilimali watu wa kutosha," amesema Dkt. Magembe.

"Pia uwepo wa Kongani Maalum la Uwekezaji Buzwagi lililopo Wilaya ya Kahama ambalo ni limetengwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji katika eneo lililokuwa Mgodi wa Buzwagi, na inatajwa kuwa tayari makampuni yameishaanza kuwekeza yakiwemo ya utengenezaji wa vipuli vya migodii, hivyo wito wangu kwa wawekezaji waje Mkoa wa Shinyanga kuna fulsa na malighafi za kutosha sana," amesisitiza Dkt. Magembe.

Kufuatia taarifa zilizotolewa na Dkt. Magembe,  Mkoa wa Shinyanga unatajwa kukua kwa kasi kubwa ya uwekezaji ambapo mpaka sasa zaidi ya miradi 900 yenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 1.6 zimesajiliwa.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRADI WA TABLET KWA SHULE ZA MSINGI WATAMBULISHWA NGAZI YA MKOA WA SHINYANGA NA WILAYA

    June 03, 2025
  • SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA, WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

    June 02, 2025
  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa