Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa avunja Serikali ya kijiji Maganzo

Posted on: January 10th, 2018

Mkuu wa Mkoa avunja Serikali ya kijiji Maganzo

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameivunja Serikali ya kijiji cha Maganzo pamoja na Kamati shule ya Msingi Jitegemee na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kukagua mapato yote na matumizi ya kijiji hicho ikiwemo fedha zilizochangwa na kutumika kujenga choo na madarasa yaliyochimbwa almasi na kufanya tathimini ya uharibifu uliojitokeza.

Mhe. Telack amefikia uamuzi huo jana wakati wa ziara yake Wilayani Kishapu, kufuatia kitendo cha wajumbe wa Kamati ya shule ya msingi Jitegemee pamoja na Serikali ya kijiji kuchimba madini kwenye vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa lengo la kutafuta Almasi. 

“Kwa utaratibu mimi ndiye mwenye mamlaka ya kuvunja Serikali ya kijiji na kuanzia leo nimesema Serikali ya kijiji hicho naivunja, tutafanya taratibu za kuchagua Serikali nyingine” amesema Mhe. Telack.

Amesema wote waliohusika wawajibike kulipa hasara hiyo kwani siyo hasara ya Serikali. Wajaze vifusi na waweke mawe ndani ya madarasa hayo kadri ya maelekezo ya wahandisi wakati taratibu za mahakama zikiendelea.

Viongozi wa kijiji cha Maganzo wanatuhumiwa kuhusika kuchimba ndani ya vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa nguvu za wananchi katika shule ya msingi Jitegemee kwa madai ya kutafuta madini ya Almasi pamoja na tuhuma nyinginezo ikiwemo kumkashifu Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Taraba kuwa hafai kuongoza Wilaya hiyo.

Wakati huo huo, Mhe. Telack amewataka matajiri wanaowatuma vijana maarufu kwa jina la “wabeshi” wanaoingia kwenye migodi kwenda kuiba mchanga wa almasi uliokwisha chimbwa kuacha mara moja tabia hiyo kwani Serikali haitawavumilia na haitawaacha imejipanga kuwakamata wote.

“Mkawaambie, wakati wao umekwisha, hatutawavumilia na hatutawaacha nadhani mshaona kazi tunayofanya kwa sasa, tuna kikosi maalumu kwa ajili ya kudhibiti wabeshi. Tutawakamata kila mmoja na kuhakikisha Maganzo ni sehemu salama ya kuishi siyo hatarishi”. Amesema Telack.

Amesema watu wote wanaotumia fedha zao kuleta uvunjifu wa amani wajue biashara hiyo imeisha kwani watapambana na Serikali, watafute shughuli nyingine za kufanya na watafute mali halali siyo kwa mtindo huo.

Amemtaka Mkuu wa kituo cha polisi Wilaya ya Kishapu awakamate wahalifu wote Maganzo wakiwemo viongozi wanaoongoza kwa uvunjifu wa Amani.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM APONGEZA USHIRIKI WA MKOA WA SHINYANGA KATIKA MAONESHO YA SABASABA.

    July 06, 2025
  • RC. MBONI ATOA WITO KWA TISEZA KUTANGAZA FURSA KUU YA KONGANI YA UWEKEZAJI BUZWAGI

    July 05, 2025
  • MHE. RIDHIWANI KIKWETE AWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA MKOA WA SHINYANGA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

    July 05, 2025
  • KATIBU TAWALA WILAYA YA KAHAMA AWAPONGEZA WASHIRIKI WA MAONESHO YA SABASABA 2025 KUTOKA MKOA WA SHINYANGA

    July 05, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa