Na. Paul Kasembo - Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amempongeza Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga No. Hilda Boniphace kwa kazi nzuri anayoifanya yeye na wasaidizi wake ya kuinua Ushirika katika Mkoa wa Shinyanga na kwamba Serikali ya Mkoa wa Shinyanga itampatia ushirikiano wakati wote huku.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo katika Hafla ya kufunga Programu ya Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD 2023) Mkoani Tabora ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein M. Bashe (MB) huku akitoa taarifa ya Mkoa wa Shinyanga kupokea Tzs. Bilioni 11.1 kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji Kata ya Nyida Shinyanga (V), kupokea mbolea Tani elfu 5, mahindi kupitia NFRA tani 2760, kuuza tumbaku kilo milioni 11.8 kwa wastani wa Dola 2.3 na kufikia Juni 2, 2023 imeuza Pamba kilo Milioni 3.9 na ununuzi unaendelea huku ikitenga Hekari 920 kuwapatia vijana wa BBT Wilayani Ushetu.
"Katika kutekeleza dhana hii ya Ushirika, nina wiwa kumpongeza sana Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace na wasaidizi wake kwa kujituma katika kazi kuinua ushirika Mkoani Shinyanga jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni anafanya kazi nzuri, nasi tutampatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi zaidi," alisema Mhe. Mndeme.
Naye Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe aliwaeleza wana Ushirika, viongozi wa Serikali, dini na wananchi waliohudhuria maadhimisho kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha wana Ushirika katika kuboresha utoaji wa pembejeo ikiwamo mbolea, dawa za mimea, vitendea kazi. Aidha Mhe. Bashe kupitia hadhara hii ametoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya Nchini kuorodhesha vijana wote wenye maeneo makubwa ya kilimo ili Serikali iwawawezeshe kupitia Ofisi hizo katika nyenzo, pembejeo lengo ni kuimarisha sektaya kilimo kwa vijana nchini.
Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniface aliishukuru sana Serikali ya awamu ya sita inayoongwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kwa nia yake ya dhati kabisaap ambapo kupitia Wizara ya kilimo imelenga kuimariaha Ushirika Nchini kwa kuimariaha usimamizi na udhibiti.
Lakini pia Serikali imempigania mkulima kwa kutoa ruzuku kwenye pembejeo na madawa ya kilimo na pia Wizara kupitia Tume ya Maendeleo ya ushirika Nchini imeendelea kuweka mipango ya usimamizi wa vyama hivi kwa kuanzisha mfumo wa Tehama wa Usimamizi wa vyama hivi unaitwa MUVU.
Bi. Hilda alisema kuwa Serikali imeleta mizani za kidigitali ili kulinda mazao ya mkulima na mwanaushirika, imeendelea kuongeza vitendea kazi muhimu kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa ushirika Mkoani kwetu na sasa tunaweza kujionea katika wiki hili la ushirika hapa Mkoani Tabora.
"Mimi kama Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Shinyanga ninae msaidia kazi Mrajis wa Vyama vya ushirika Nchini, na amabye Msimamizi ngazi ya Mkoa kwa kushirikiana na viongozi wangu wa Serikali ya Mkoa katika kuunga mkono jitihada hizi ambazo zinafanywa na Serikali chini ya Mhe. Waziri wa kilimo nitahakikisha ninafanya kazi yangu ya usimamizi kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha ushirika wetu unaimarika, kurudisha heshma ya ushirika kwa kuhakikisha vyama hivi vinatekeleza madhumuni ya kuanzishwa kwake kwa kuzingatia sheria , kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na TCDC," alisema Hilda.
Hilda alisema katika kulitekeleza hili tunahitaji zaidi viongozi wa ushirika wenye nia njema na vyama hivi ambao kupitia kazi zao watasaidia wanaushirika na wananchi wengine walio nje ya ushirika kutamani kujiunga na ushirika kutokana na huduma mbalimbali ambazo wao kama viongozi wanapaswa kuwahudumia wanachama wake ili lengo la kuinua uchumi wa mwanachama mmoja mmoja liweze kuonekana.
Ninazidi kuhamasisha wananchi mbalimbali wenye shughuli za kiuchumi waweze kujiunga na ushirika ili kupitia umoja wao wataweza kuyatatua matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayowakabili kwani ushirika ndio nyenzo pekee ya kuimariaha uchumi kwa wenye kipato cha chini.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa