Waziri wa TAMISEM Mhe. Mohamed Mchengerwa (MB), amekabidhi magari manne kwa ajili ya Usimamizi katika Sekta ya Afya Mkoani Shinyanga ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa Waganga Wakuu wa wilaya na Mkoa tukio ambalo limefanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga na kushuhudiwa na viongizi mbalimbali kutoka TAMISEMI na kwa upande wa shinyanga wameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme.
Mhe. Mchengerwa amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Yudas Ndungulile na Waganga Wakuu wa Halmashauri, kuyatumia kikamilifu kuwatembelea Watumishi wa Afya pamoja na kufanya nao vikao vya mara kwa mara, ili kuboresha utendaji kazi wa kuhudumia wananchi na kuokoa afya zao, wakiwamo wajawazito na kupunguza vifo vya uzazi huku akitumia muda huo kuwataka watumishi katika nafasi zao kufanya mikutano na wananchi ili kuwaelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita.
“Nakabidhi Magari haya Manne ya usimamizi katika Mkoa wa Shinyanga ambapo gari moja ni la Mganga Mkuu wa Mkoa, na Mengine Matatu ni ya Waganga Wakuu wa wilaya, hivyo yatumieni Magari haya kwenda kufanya vikao na watumishi na kukagua huduma za afya ili wananchi wapate huduma bora za matibabu,”amesema Mchengerwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma za na sekta nyingine kwa kutoa fedha nyingi na kujengwa Vituo vya Afya, Zahanati,Hospitali za Wilaya, Mkoa, kutoa Vifaa tiba, Madawa, na sasa ameleta Magari Manne ya usimamizi kwa Waganga Wakuu huku akisema mkoa wa shinyanga Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameivifikia vijiji vyote 506 koani shinyanga kupitia sekta mbalimbali hivyo wanashinyanga wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza sana.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa