Na. Paul Kasembo, SHY RS.
AFISA Ushirika kutoka Ofisi ya Mrajis Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Ngd. Deogratous Momburi amefunga mafunzo na kugawa vyeti kwa washiriki kutoka kwa viongozi wa Vyama Vya Ushirika vinavyojihusisha na Mazao ya Mbogamboga Shinyanga huku akiwasisitiza kwenda kuhamasishana na kuanzisha vyama vingine vingi zaidi ili ifike wakati waweze kuanzisha Chama Cha Ushirika Kikubwa zaidi na ikiwezekana kwa mwaka 2025 waweze kuibuka washindi kwenye Jukwaa la Ushrika.
Momburi ameyasema katika hafla ya ufungaji iliyofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Lyakale Hotel ambapo pamoja na mambo mengine wasiriki wamekumbushwa kwenda kuyatumia vema mafunzo haya na taaluma walizozipata katika kuimarisha na kuboresha kazi zao ikiwemo ya uandishi wa vitabu na utunzaji wa kumbukumbu hasa za fedha katika kudhibiti matumizi.
"Katumieni elimu na taaluma hii mliyoipata hapa katika mafunzo haya ya siku mbili katika kuimatisha utendaji kazi na kuboresha shughuli zenu za kila siku ikiwemo katika Uandiahi wa Vtabu na Uunzaji wa Kumbukumbu za Fedha sanjari na kwenda kuhamasisha na kuanzisha vyama vya ushiriki vingine ili ifike wakati muweze kuanzisha Chama kikubwa zaidi," amesema Momburi.
Momburi ambaye alimuwakilisha Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushiriki Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace amesema kuwa, Mrajis ameendelea kusisitiza kwamba Serikali inayo nia njema ya kuimarisha Vyama hivi vya Ushirika ili ziwe Imara zaidi na baadae ziwe kimbilio la wananchi walio wengi huku akisema kuwa vyama hivi vilivyopata mafunzo viende kuwa vya mfano wa kuigwa na kutafsiri kwa ufasaha Sheria za Ushirika zinavyoelekeza.
Kwa upande wake ndg. Justine Mallo kutoka COASCO ametoa wito kwa washiriki wote kwenda kuwa wajumbe na walimu wazuri ili kuimarisha vyama vya ushirika kwa kuanzisha vingi zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake Bi. Laurencia Makwalwe ameishukuru sana Serikali na Wadau wote kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo haya ambayo yamewaongezea uelewa na maarifa katika utendaji kazi wao wa kila siku na kwamba watakwenda kuwahamasha wenzao kuanzisha Vyama zaidi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa