Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela, amekabidhi Mwenge wa Uhuru mapema leo tarehe 14 Mei, 2019 kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Christopher Derek Kadio baada ya kukamilisha mbio katika Mkoa wa Shinyanga.
Msovela amesema kuwa, Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani hapa umeweza kupitia jumla ya miradi ya maendeleo 53 yenye thamani ya shilingi 47,517,967,547 ambayo imechangiwa na Serikali Kuu, Halmashauri, Wananchi na Wahisani katika sekta za Maji, Afya, Elimu, Kilimo, Mifugo na Mazingira.
Pamoja na miradi hiyo, pia Mwenge wa Uhuru umepitia na kuona jitihada mbalimbali za Mkoa wa Shinyanga za kudhibiti Rushwa, UKIMWI, Malaria na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo kushuhudia upimaji wa hiyari wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ambapo jumla ya wananchi 3836, wanaume wakiwa ni 2508, na wanawake 1228,walipima. Waliokutwa na maambukizi ni 49 sawa na asilimia 1.3
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Bw. Mzee Mkongea Ally pamoja na wenzake wametoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru Mwaka huu 2019 kwa wananchi katika kila Halmashauri ya Wilaya, Mji na Manispaa ambao ni “maji ni haki ya kila mtu, tuvitunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa kutoka Mkoa wa Geita hapo tarehe 08 Mei, 2019 na kukimbizwa katika Wilaya zote tatu za Kahama, Shinyanga na Kishapu hadi tarehe 13 Mei, 2019.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa