Na. Paul Kasembo, KAHAMA
MWENGE wa Uhuru ukiongozwa na ndg. Godfrey Mnzava umezindua upanuzi wa mradi wa skimu ya maji kutoka Zogomera hadi Nyandekwa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama huku akiwapongeza Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA) kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wanayafsiri maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwatua ndoo akinamama kichwani na pia kuwaondelea adha wananchi ya ukosefu wa majisafi na salama.
Akitoa taarifa ya mradi Meneja wakala wa maji vijijni (RUWASA) Wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili amesema wameutekeleza kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA)na sasa upo chini ya Kuwasa huku akieleza kuwa mradi ulianza kutekelezwa februari 2022,na kukamilika januari 2024, na umewafikia wananchi 9,268 kati ya 16,375 wa Kata ya Nyandekwa, kutoka katika vijiji vya Lowa, Buduba, Bujika na Nyandekwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa