Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MWEZESHAJI kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vga Siasa Tanzania ndg. Frank Shija amewaomba Viongozi wa Vyama vya Siasa wilayani Shinyanga kwenda kuzisoma vizuri Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania @orpptanzania kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 huku akiwakumbusha kutanguliza uzalendo pia katika utekelezaji wa majukumu yao hasa wanapoelekea kuanza kampeni.
Shija ameyasema haya leo tarehe 22 Oktoba, 2024 alipokuwa akizungumza na Viongozi katika Wilaya ya Shinyanga inayounganisha Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amewapatia wajumbe vitabu vya Sheria hizo na amewaomba ushirikiano wao kwa kipindi ambacho watakuwa hapa mkoani Shinyanga.
Akifungua mafunzo haya, Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga amewaomba kwenda kufanya kampeni na kutangaza Sera za Vyama vyao kwa ustaarabu, kuwa wazelendo, kupendana, umoja, kushirikiana na kuacha kutuhumiana kwa mambo yasiyokuwa na ukweli kwani kuna maisha yataendelea baada ya uchaguzi.
Aidha, wajumbe wa mafunzo haya wamekiri kupokea vitabu vyenye kuelezea Sheria hizi huku wakiahidi kwenda kuzipitia kwa umakini huku wakiiomba Ofisi ya Msajili kuwa karibu nao zaidi ukizingatia kuwa kipindi hiki ni cha kuelekea kampeni kuanza kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo wamesema huwa kuna sintofahamu kadhaa huwa zinajitokeza kwa hiyo uwepo wa wawakilishi hawa kutasaidia sana.
Kando nao, Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze na Dkt. Kalekwa Kasanga wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa nyakati tofauti wamewashukuru sana viongozi wa Vyama vya Siasa wilayani Shinyanga kwa namna ambavyo wamekuwa wakiwapatia ushirikiano wakati wote
Novemba 27, 2024 ni siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo wananchi watapata nafasi ya kuchagua viongozi wao wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji ambao watawahudumia kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa