Na. Shinyanga RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga amewataka viongozi wa Baraza hiki jipya kuja na ubunifu zaidi ikiwemo kufuatilia, kushughulikia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto na masuala yote yahusuyo watumishi sanjari nankuwasilisha kwenye Menejimenti.
Haya yamesemwa leo tarehe 11 Machi, 2024 wakati wa kikao cha Baraza hili ambapo pamoja na maelekezo haya kwa uongozi mpya lakini pia amewaeleza watumishi wote kuwa na uzalendo, kutanguliza uzalendo na kuishi katika uzalendo wakati wote wanapokuwa wanahudumia jamii yetu, huku akisisitiza watumishi kutumia vema Baraza hili katika kuwasilisha masuala yao ya kiutumishi.
"Nitumie nafasi hii kuwataka viongozi wapya wa Baraza la Wafanyakazi kuja na ubunifu wa kazi zao ikiwemo kufuatilia, kuwasilisha na kutatua changamoto zinazowahusu wajumbe wa Baraza na mkatangulize zaidi uzalendo wakati wote mnapokuwa mnahudumia wananchi wetu," amesema Prof. Siza.
Kando na hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ambaye hakuwepo, Prof. Siza amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa na imani nao katika kumsaidia kazi hapa Mkoani Shinyanga na kuahidi kutumikia jamii kwa nguvu na weledi mkubwa zaid.
Baraza la Wafanyakazi ini chombo cha mawasiliano na ushauri ambacho viongozi na wafanyakazi hukaa pamoja na kuzungumzia mpango kazi na uchumi wa taasisi yao na kutathimini ufanisi na tija baada ya kupanga na kutekeleza mipango ya taasisi.
Wafanyakazi hupata fursa ya kutoa maoni, changamoto na kushiriki na kushirikishwa katika mchakato wa uendeshaji wa taasisi yao.
Kwa uwazi na uhuru wote, wajumbe wamemchagua Ndg. James Maligisa kuwa Katibu na Naibu Katibu ni Ndg. Angel Silayo ambapo wamewashukuru wajumbe na kuwaahidi kuwatumikia kwa dhati na bila upendeleo wowote.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa