• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RAIS DKT. SAMIA ATOA ZAWADI KWA MAKAO YA WATOTO NA MAKAZI YA WAZEE - SHINYANGA

Posted on: March 30th, 2025

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MHE. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali kwa Makao ya Watoto Yatima (Shinyanga Society For Orphans) iliyopo Bushushu na Makazi ya Wazee na  Wenye Mahitaji Maalum Kolandoto iliyopo Kata ya Kolandoto zote zikiwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza baada ya kukabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa ikiwa ni kuelekea katika Sikukuu ya Eid Al - Fitr, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua, anathamini na kuheshimu uwepo wa wao na kwamba yeye mwenyewe na Serikali yake anawapenda na kuwajali wakati wote ndiyo sababu ya kuwapelekea zawadi hizo kwani wao pia ni jamii kama ilivyo jamii nyingine na wanazo haki sawasawa kama binadamu wengine.

"Tunapoelekea katika kuhitimisha Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhan, nimeelekezwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niwaletee zawadi zake alizotoa maalum kwa ajili yenu ili katika kusherehekea Sikukuu hii ya Eid Al-Fitr muweze kufurahi pamoja naye kupitia zawadi hizi," alisema RC Macha.

"Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua, anathamini na kuheshimu uwepo wenu na kwamba Serikali anayoiongoza itaendelea kuwa karibu na kuishi nanyi wakati wote, aidha itaendelea kusaidizana nanyi katika nyanja na nyakati mbalimbali kutegemea na mahitaji ya wakati husika pia," alisisitiza RC Macha.

Kwa nyakati tofauti Mkurugenzi wa Makao ya Watoto Bibi Haiyamu Said na Msimamizi wa Makazi ya Wazee na Wenye  Mahitaji Maalum Bi. Sophia Kang'ombe wamemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini, kuwajali na hata kuwapatia zawadi mbalimbali nyakati zote kupitia wasaidizi wake (Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga) na kwamba wao wanamuombea kwa Mwenyezi Mungu awe na afya njema wakati wote ili andelee kuwahudumia wao na Watanzania wote.

Huu ni muendelezo na utaratibu wake Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kutoa zawadi na mahitaji mbalimbali kwa makundi mbalimbali ambapo kwa leo Makao ya Watoto Yatima (Shinyanga Society For Orphans) chenye jumla ya watoto 23 huku Makazi ya Wazee na Wenye Mahitaji Maalum Kolandoto.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRADI WA TABLET KWA SHULE ZA MSINGI WATAMBULISHWA NGAZI YA MKOA WA SHINYANGA NA WILAYA

    June 03, 2025
  • SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA, WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

    June 02, 2025
  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa