Na. Paul Kasembo, SHY DC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa Sikukuu ya Pasaka kwa Makazi ya Wazee na Wenye Mahitaji Maalumu Usanda yaliyopo Halmasahuri ya Wilaya ya Shinyanga na Makao ya Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Hatarishi ya Beauty for Ashes yaliyopo Kitangiri Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu pamoja nao..
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Bi. Lydia Kwesigabo ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha alisema kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaagiza kupeleka zawadi hizo kwa wazee na watoto hao ili kuwashika mkono katika kusherehekea Sikukuu na kwamba anatambua, anathamni, anaheshimu na anawajali sana wao kama sehemu ya jamii na kwamba wao pia kama walivyo watoto na wazee wengine wanazo haki na stahiki sawa.
"Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, mimi pamoja na watumishi wenzangu tumekuja hapa kuleta zawadi zilizotolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka pamoja naye ambapo ametupatia vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Mafuta ya Kupikia, mboga (mbuzi), Sharubati (juice), sabuni,mafuta ya kujipaka, wipers. pampers na maziwa kwa watoto hawa wachanga hivi vyote tumeagizwa tuwaletee na pia ametoa salamu zake kwenu kuwa anawapenda sana na yupo pamoja nanyi," alisema Lydia.
Huu ni muendelezo wa utoaji zawadi kwa Makao na Makazi [9) mbalimbali hapa mkoani Shinyanga, ambapo awamu ya kwanza zawadi zilitolewa ikiwa ni wakati wa kuelekea Sikukuu ya Eid Al - Fitr na sasa ni kuelekea Sikukuu ya Pasaka.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa