Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni aitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu Bi. Irene Mlola kuandaa namna bora itakayo wakutanisha wao na wadau wa mazao ya kilimo mkoani Shinyanga ili waweze kupata nafasi ya kuwasilisha mipango yao, kupokea, kujadili na kupata maoni ya wajumbe kwa muktadha mkubwa wa utekelezaji wa majukumu ya COPRA katika Sekta ya kilimo.
RAS CP. Hamduni ameyasema haya leo tarehe 9 Januari, 2025 alipokutana na viongozi hao wa COPRA ofisini kwake ambao walifika kwa lengo la kujitambulisha pamoja na kuelezea wajibu na majukumu yao ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri lakini pia ametaka kuwa na mkakati endelevu wa utoaji elimu kwa wadau.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa COPRA Bi. Irene pamoja na kumshukuru RAS CP. Hamduni kwa mapokezi na ushirikiano aliowapatia tangu walipowasili huku akimuahidi kulitekeleza agizo lake kwa kuandaa na kufanya mkutano ambao utawakutanisha na wadau wa Sekta ya Kilimo tarehe 24 Januari, 2025.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa