Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekabidhi vitendea kazi ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma hapa mkoani Shinyanga huku akisisitiza utunzaji wa vitendea kazi hivi ambavyo Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI imetoa magari manne (4) ya wagonjwa (Ambulance), gari la chanjo moja (1) na pikipiki kumi (10).
RAS CP. Hamduni amekabidhi leo tarehe 2 Januari 2025 kwa Faustine Mlyutu ambaye ni muwakilishi wa Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Daktari Yudas Ndungile pamoja na Waganga Wakuu wa Halmashauri na kumshukuru sana Mne. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha utoaji huduma mbalimbali katika jamii ikiwemo afya.
"Kwa niaba ya Serikali ninawakabidhi vitendea kazi hivi ikiwa ni magari 4 ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Halmashauri ya Shinyanga DC, Kishapu DC, Msalala DC na Ushetu DC, gari 1 la Mkoa kwa ajili ya kusambaza Chanjo na pikipiki 10 kwa Kahama MC 1, Msalala DC 2, Shinyanga DC 2, Kishapu DC 1, Ushetu DC 1 na Shinyanga MC 1. Aidha nitumie nafasi hii kutaka kwenda kuhakikisha vifaa hivi vinatunzwa kwa maslahi makubwa ya wananchi wetu na Taifa kwa ujumla," amesema RAS CP. Hamduni.
Huu ni muendelezo wa dhamira ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha inaboresha, kulinda na kuimarisha afya za wananchi wake sanjari na kusimamia na kutafsiri maono ya Mhe. Rais kwa vitendo kupitia Sekta mbalimbali ambapo Mkoa wa Shinyanga takribani Vijiji vyote 506 vinavyounda Mkoa vimefikiwa na miradi ya maendeleo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa