Na. Paul Kasembo, KAHAMA.
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha ameongoza zoezi la ugawaji wa zawadi za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwenye makao ya kulelea watoto yatima ya Mvuma yaliyopo Kata ya Nyasubi, Manispaa ya Kahama huku lengo ni kuwafanya watoto hawa waweze kusherehekea sikukuu kwa amani, umoja na upendo kama watoto wengine.
RC Chacha ameongoza zoezi hili leo tarehe 27 Desemba, 2024 ambapo pamoja na mambo yote amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kutoa zawadi hizi ili watoto wanaotunzwa katika makao ya kulelea watoto yatima waweze kuona wanastahili kuthaminiwa na kupendwa kama watoto wengine katika familia.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nia ya dhati ameamua kutoa zawadi hizi kwenye vituo vya kulelea watoto yatima ili na wao pia waweze kuona wanathaminiwa na kupendwa kama watoto wengine katika familia” amesema RC Chacha.
Akitoa taarifa ya kituo cha Mvuma Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masoud Kibetu ameeleza kuwa kituo hiki kinasimamiwa na Manispaa ambapo kinawawezesha watoto hawa kwa mahitaji mbalimbali kama chakula na elimu huku akiishukuru Serikali kwa msaada huu kwani watoto hawa wanauhitaji sana ili waweze kuishi kwa furaha.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa