Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 20 Desemba, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Umoja wa Makanisa yenye Huduma ya Mtoto yanayoshirikiana na Shirika la Compassion ambayo yana jumla ya vituo 14 mkoani Shinyanga ambapo amewaahidi kuendelea kushirikiana nao katika mambo yote na kuwaasa waendelee kufanya kazi ya Mungu bila kuchoka.
Umoja wa Makanisa yenye Huduma ya Mtoto unatarajia kuanzisha kampeni ya miezi 6 ya kupinga ndoa na mimba za utotoni katika Wilaya ya Shinyanga na Kahama, kampeni ambayo itazinduliwa tarehe 31 Januari, 2025 na kuhitimishwa tarehe 16 Juni, 2025 katika Wilaya ya Kahama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa