Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amelipongeza Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Ukanda wa Dhahabu (NGBF) ambalo linaendesha Semina ya Familia, Malezi, Biashara na Huduma za Afya hapa Shinyanaga na kuwataka waumini wote kuendelea kumuombea kwa Mungu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili aendelee kuwatumikia wananchi wote na kuwaletea maendeleo.
Haya yamesemwa katika Ufunguzi wa Semina hii ambayo inajumuisha waumini wa Kisabato na wasiokuwa wasabato kwa lengo kupata jamii iliyo bora zaidi yenye upendo wa dhati kuanzia familia, yenye malezi yasiyokiuka mmomonyoko wa maadili, yenye kujenga jamii ambayo itakuwa na taaluma ya ujasiliamali na kuzingatia afya bora.
"Kwa dhati ya moyo wangu, nimefurahishwa na maandalizi ya semina hii pamoja na dhamira yake, kwakuwa Taasisi za zinao uwezo mkubwa zaidi wa kuijenga jamii yenye malezi na makuzi mema katika familia zinazofuata na kuzingatia afya bora na hivyo ninyi Waadventista Wasabato Shinyanga ni mfano wa kuigwa katika hili, nawapongeza sana," amesema RC Macha.
Serikali inailea na kuitunza jamii hasa vijana kwa kuwawezesha katika Sekta ya Elimu, Uchumi, Amani nk ambapo nanyi Taasisi za Dini mnawawezesha kiroho na katika mafundiaho ya Mwenyezi Mungu ili waishi kwa kwa kumpendeza Mungu na watende haki katika jamii wanazoishi nazo.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Ukanda wa Dhahabu alimshukuru sana RC Macha kwa kuridhia kuja kufungua Semina hii muhimu kwa muktadha wa vijana na wanajamii wote wa Ukanda wa Dhahabu, akamuahidi kwa yote aliyoyasema wameyapokea na mwisho akamuomba aridhie tena kuja kufunga Semina hii tarehe 27 Aprili, 2024.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa